Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ameshiriki maadhimisho ya miaka 30 tangu kutokea kwa mauaji ya Kimbari ya mwaka 1994 dhidi ya Watutsi.  Maadhimisho hayo yamefanyika tarehe 07 Aprili, 2024  katika Makumbusho ya Mauaji ya Kimbari, yaliyopo  Kigali  Nchini Rwanda,  ambapo  Viongozi kutoka nchi mbalimbali wakiongozwa na Mhe. Paul Kagame, Rais wa Jamhuri ya Rwanda  wameshiriki pia. Pamoja na mambo mengine Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan  ameweka shada la maua kwenye makaburi.